NAIBU WAZIRI MUSSA SIMA AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYA YA CHEMA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima hii leo amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya cha Chemba katika eneo la Farkwa kuijionea athari za ukataji miti kwa matumizi ya kuchomea tofali na mkaa. Katika ziara hiyo

Naibu Waziri amemuagiza Meneja wa Wakala wa Misitu (TFS) – Dodoma kukaa na Uongozi wa Wilaya ya Chemba ili kuainisha na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya hifadhi na uvunaji wa misitu na si kuvuna kiholela kama inavyofanyika hivi sasa. Pia, Naibu Waziri ametoa rai kwa Mikoa mingine kuainisha maeneo ya Hifadhi ili yaweze kutangazwa kama maeneo lindwa