MKUTANO WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI MAURITANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema “Tanzania chini ya Serikali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli inajitahidi sana kupambana na rushwa pamoja na viashiria vyake”

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakatiwa kujadili Kauli mbiu ya Umoja wa Afrika kwa mwaka 2018 “Kushinda Vita dhidi ya Rushwa: Njia endelevu ya mabadiliko ya Afrika”katika Mkutano wa kawaida wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaomalizika leo mjini Nouakchott, Mauritania.

Makamu wa Rais amesema rushwa inaumiza watu hususani watu masikini nakudhoofisha ukuawaji wa uchumi hivyo ni vyema rushwa ipingwe kwa nguvu zote.

Aidha, Makamu wa Rais amesema Tanzania inatambua vita dhidi ya Rushwa ina hitaji jitihada za pamoja katika ngazi zote ikiwemo Kitaifa, Kikanda na Bara zima.

Katika mkutano huo ambao umejadili mambo mbalimbali, Tanzania itaendelea kushiriki katika kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo