Mhe. Samia amuwakilisha Rais Magufuli mkutano wa AU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Julai 07, 2019 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 12 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali kuhusu Eneo Huru la Biashara Afrika (AFRICAN CONTINENTAL FREE TRADE AREA-AFCFTA).

Mkutano huo unaofanyika mjini Niamey Nchini Niger umefunguliwa na Mwenyekiti wa AU Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri.