Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu ahudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) katika mji wa Nouakchott, Mauritania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu leo amehudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) katika mji wa Nouakchott, Mauritania.

Pamoja na mambo mengine mkutano huu umejikita katika masuala ya Kupambana na Rushwa katika bara la Afrika, Mkakati wa Biashara ya Pamoja, masuala ya Ulinzi na Amani katika nchi za Congo DRC, Burundi na Sahara Magharibi, pamoja na kujadili masuala ya mabadiliko yatakayoleta tija katika Utawala na kuboresha uchumi.

Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Katika hotuba ya Ufunguzi wa mkutano huo, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais wa Rwanda Paul Kagame alisemaKama umoja, tupo pamoja na watu Ethiopia na Zimbabwe, kufuatia mabadiliko ya kisiasa ya amani.Tunashutumu mashambulizi yaliotaka kuvuruga amani na tunatoa pole kwa waliopoteza maisha”.

Kagame amesema pia wameridhishwa na hatua zinazoendelea za kuleta Amani Sudani ya Kusini. Mkutano huo unatarajiwa kumalizika kesho ambapo kuna uwezekano mkubwa Viongozi hawa wa Afrika watakutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa chakula cha mchana.