MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA ANOGESHA SIKU YA WAKIZIMKAZI (KIZIMKAZI DAY)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaomba Wazee wa Kizimkazi kukubali na kuwabariki vijana kwenda kujifunza taaluma na elimu mbalimbali za kuendeleza miradi ya kimaendeleo katika Vijiji vya Kizimkazi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo kwenye kilele cha Siku ya wa kizimkazi iliyofanyika Kizimkazi Mkunguni, wilayayaKusini, Mkoa wa Kusini Unguja. Sherehe hizo hufanyika kila mwaka na zenye lengo la kuhamasisha Umoja, Mshikamano na Ushirikiano, mwaka huu sherehe hizo zimebeba ujumbe unaosema“ UmojaWetu, Ushirikianowetu, naMshikamanowetundiongaoyetu”

Makamu wa Rais ametoa wito kwa Vijana watakaopata fursa ya kujifunza taaluma mbalimbali za maendeleo kurudi nyumbani kujenga nchi. Katika Sherehe za mwaka huu ngoma ya asili ya Kizimkazi inayojulikana kama Shomoo ilikuwa kivutio kikubwa, mchezo wa kuvuta Kamba kwa wanawake na wanaume, mchezo wa Mabofu (kupasua puto) kwa watoto na vyakula vya asili vya watu wa kizimkazi vilipendezesha sherehe hizo.

Sambamba na burudani hizo pia zilifanyika shughuli za kimaendeleo zikiwemo Uzinduzi wa nyumba ya Daktari na nyumba ya walimu pamoja na ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Shehiya ya Kizimkazi Dimbani. Makamu wa Rais amewashukuru wadhamini wa mwaka huu katika shughuli za maendeleo ambao ni Sport Pesa na Kampuni ya Multichoice DSTV kwakuwezesha kujenga nyumba ya madaktari na walimu.

Akisoma risala ya wananchi wa Kizimkazi, Mwalimu Said Ramadhani Mgeni amesema dhamira ya wananchi kuweza kubuni mambo mbalimbali kwa kutumia rasilimali zilizowazunguka ili waweze kujikwamua kiuchumi na maendeleo ili kufikia malengo waliyojiwekea na yale yaliyowekwa naTaifa.

Sherehe hizo zimehudhuliwa na Waziri wa Sheria na Utawala Bora Zanzibar  Mhe. Haroun Suleiman, Waziri waVijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ali Abeid Karume, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib Hassan pamaoja na viongozi wegine wa Chama na Serikali.