MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA SIKU LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MALAWI MKOANI MBEYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Tanzania pamoja na Malawi zimetambua umuhimu wa kuimarisha biashara za mipakani ambao pia ni mkakati wa Viwanda wa SADC na mpango wa ushirikiano wa kikanda.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Sikumbili la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi lililofanyika mkoani Mbeya.

Makamu wa Rais amesema kongamano hili litawezesha kuzungumzia fursa na changamoto baina ya nchi hizi mbili kufanya biashara rasmi ambapo wafanyabiashara watatambuliwa na kufuata taratibu za nchi mbili na kulipa kodi za serikali.

“Kwa zaidi ya miaka sita biashara kati ya Tanzania na Malawi imekuwa na utendaji thabiti. Jumla ya kiasi cha mauzo ya nje ya Tanzania hadi Malawi kwa miaka sita kutoka 2011 hadi 2016 ilikuwa 700, 525 tani na thamani ya dola 305.3 milioni wakati kiasi cha uagizaji kutoka Malawi hadi Tanzania kwa kipindi hicho kilikuwa na tani 328,335 na jumla ya dola milioni 244.5 milioni” Amesema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kupitia Kongamano hili anaami ni kiasi na thamani ya biashara kati yetu itakuwa na uwezo wa kuimarishwa na kuongezeka kwa sekta kubwa ya viwanda na kilimo katika nchi zote mbili.

Aidha Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii wa Nchi ya Malawi Mhe. Henry Mussa (MB) amesema leo imeandikwa historia kubwa kati ya nchi hizi mbili na anaamini Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya nchi hizi mbili litakuja na majibu ambayo yatasaidia kukuza uchumi wa pande zote.