Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani chafanyika Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wangazi zote kuongeza nguvu katika utekelezajiwa Sera, Sheria, Mikakati na miongozo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Makamu wa Rais wa ameyasema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho   ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja.

“Ni muhimu,mipango ya maendeleo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira ili nchi yetu iwe na maendeleo endelevu” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kazi ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa hifadhi ya mazingira unahitaji ushirikiano wa wadau wote kwa ngazi zote.

Maadhimisho ya Kimataifa yanafanyika India katika mji wa New Delhi ya kubeba ujumbe wa kuhimiza kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na matumizi ya bidhaa za plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini hapa nchini Kitaifa ujumbe wa maadhimisho ni “Mkaa Gharama: tumia Nishati Mbadala”

Mapema leo,Makamu wa Rais alizindua ukuta wa bahari uliopo kwenye barabara ya Barack Obama wenye urefu wa mita 920, ukuta huo ambao umejengwa kuzuia bahari kuingia nchi kavuu inakadiriwa kuwa na maisha kati ya miaka 70 mpaka 100 kutoka sasa.

Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya Awamu yaTano imedhamiria kujenga uchumi wa Viwanda nazipo faida nyingi za hifadhi na usimamizi zitakazotokana na Tanzania kuwa na Viwanda.

Mwisho, Makamu wa Rais amesema katika kufanikisha suala zima la uhifadhiwa Utunzaji wa mazingira ni lazima tuifanye kila siku iwe siku ya Mazingira.