KASCO YAAGIZWA KUFANYA THATHMINI YA ATHARI KWA MAZINGIRA

[:en]Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mussa Sima (mwenye tai) akitoa maelekezo ya kazi mara baada kutembelea eneo la Mundemu, Kata ya Mundemu Wilayani Bahi ambapo mwekezaji wa Kampuni ya Kasco Limited anayejishughulisha na ujenzi wa Kiwanda cha kuponda kokoto ametakiwa kufuata takwa la Kisheria la kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira, na kumtaka mwekezaji huyo ndani ya siku saba kuonana na Wataalamu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kupewa utaratibu wa kufuata.[:]