FAQs

Is it compulsory for a Vice President to be obtained from Zanzibar all time?

It is not compulsory for the Vice President to be obtain from Zanzibar all time. The Vice President obtain from running mate of winning Political Party on Presidential election

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Muungano wa Nchi huru mbili zilizojulikana kama Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Nchi hizi mbili ziliingia kwenye Mkataba wa Muungano mnamo tarehe 22 Aprili, 1964 na kuwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia tarehe 26 Aprili, 1964. Muungano huu ni wa serikali mbili, yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) inayoshughulikia mambo yote ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inayoshughulikia mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanzania Zanzibar.

Mkataba wa Muungano ulitiwa sahihi na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume tarehe 22 Aprili, 1964 huko Zanzibar.  Mkataba huo ulithibitishwa tarehe 26 Aprili, 1964 na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam na kubadilishana hati za Muungano. Sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano kwamba:

“Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za Muungano)

Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” lilibadilishwa baadae na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.

Kuna maeneo mangapi ya Muungano na ni yapi?

Maeneo ya Muungano yapo 22 kama yalivyoorodheshwa katika nyongeza ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni kama yafuatayo:-

1.Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ;

2.Mambo ya Nchi za Nje ;

3.Ulinzi na Usalama;

4.Polisi;

5.Mamlaka juu ya mambo yanayohusikana na hali ya hatari;

6.Uraia;

7.Uhamiaji;

8.Mikopo na biashara ya Nchi za Nje ;

9.Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano;

10.Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa
bidhaa  zinazotengenezwa  Nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha;

11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu;

12.Mambo yote yanayohusika na sarafu, fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti),
mabenki ( pamoja na mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;fedha za kigeni na
usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni;

13.Leseni za Viwanda na Takwimu ;

14.Elimu ya Juu;

15.Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano ;

16.Maliasili ya Mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na Gesi asilia ;

17.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo ;

18.Usafiri na usafirishaji wa anga ;

19.Utafiti;

20.Utabiri wa Hali ya Hewa;

21.Takwimu;na

22.Uandikishaji wa Vyama vya Siasa na mambo mengine yanayohusiana na hayo.